Ya Moto Lyrics
- Genre:Afrobeat
- Year of Release:2022
Lyrics
Ya Moto - Nino Tz
...
(Mmmh, they call me Nino, ahh)
Upele ushaniota nami kucha sina, naambulia tu maumivu
Kuendekeza wivu sili nikashiba, kaa lishageuka majivu
Nyota ya punda niliambulia fimbo, ona naumizwa mwenyewe
Mi kinda lako ukanila kwa lindo, kesi ukamwachia mwewe
Siri sirini mapenzi tuliahidiana (aaaah)
Ukaanika juani ya ndani wakagawana (aaah)
Hesabu za kutoa mwenzangu ukagawanya (aaah)
Nimeambulia sufuri, ona mwenzako nishafeli
Inaunguza sitaki
Yamoto, yamoto mapenzi (hata siwezi kuyauguza)
Yamoto, yamoto mapenzi (mi yashaniunguza)
Yamoto, yamoto mapenzi (nayaogopaa)
Yamoto, yamoto mapenzi (mm mmmh)
Painamapo ndo painukapo, kutendwa sio kilema
Leo kulia kwangu, kesho kwako, kariri nayosema
Na, sifichi mi, mwenye dhiki acha nkatafute wa kunipenda
Na sisiti si-lalamiki sa umeridhika unaweza kwenda
Huenda zi-mbichi ha-ziridhishi ndo mana hukudiriki kunipenda ah
Sifichi japo ntakumiza'ila ntajimiliki siku z'takwenda aaah,
Siri sirini mapenzi tuliahidiana (aaaah)
Ukaanika juani ya ndani wakagawana (aaah)
Hesabu za kutoa mwenzangu ukagawanya (aaah)
Nimeambulia sufuri, ona mwenzako nishafeli
Inaunguza sitaki
Yamoto, yamoto mapenzi (hata siwezi kuyauguza)
Yamoto, yamoto mapenzi (mi yashaniunguza)
Yamoto, yamoto mapenzi (nayaogopaa)
Yamoto, yamoto mapenzi (mm mmmh)
Mmmh, mmmh
Kwani so nilikubali 'meza kaa la moto, ili walau npate ahueni, ila mapenzi kwangu ni changamoto basi yafunzwe ata shuleni Memkwa ntasoma..