Tiririka Acoustic Lyrics
- Genre:Afropop
- Year of Release:2023
Lyrics
Tiririka Acoustic - Yammi
...
Mapenzi yanenibadilisha sikuhizi sinaga ubaabe
Nishakua guta mniache moyoni niyabebe baby
Mi nikuku wako ukitaka mayai niyatage sema
Naujinga we nisitiri husinibwage
Baby matamanio nishatupaga huko
Sintolivua vazi la heshima ulonivisha kwa upendo
Sina matarajio yakuondoka kwako
Dunia imeshabadili wengi wakawa vituko
Mapenzi sio mchezo wa ngumi
Nipige na khanga au ukuni
Ata ukinifinya finya haiumii naona rahaa
Naisoma namba kwa kirumii
Huu mchezo gani mbona wakihuni
Ata ukinifinya finya haiyumi ah naona rahaa
Umenijaza upendo mpaka unanitirirka
(Tiririri)
Aahh unanitiririka (tiririri)
Tiri tiri riri riri riri (tiriririri)
Upendo unanitiririka miee (tiriririri)
Tiririririri
........
Natiririririka kama si jaba najaza ndoo
Raha anazonipa naitika marhaba nikipa shikamoo
Aniachi njiani nafika mi kwake yes sisemi no
Siwezagi kususa nisipomuona wafukuta moyo
Asante angalau umenionesha maana ya upendo
Na sio kwa nahau umenionesha kwa vitendo
Sitokaaga nisahau nilinyanyasika hapo mwanzo
Niliyaoga madharau kwa kumpenda asojali upendo
Mapenzi sio mchezo wa ngumi
Nipige na khanga au ukuni
Ata ukinifinya finya haiumii naona rahaa
Naisoma namba kwa kirumii
Huu mchezo gani mbona wakihuni
Ata ukinifinya finya haiyumi ah naona rahaa
Umenijaza upendo mpaka unanitirirka
(Tiririri)
Aahh unanitiririka (tiririri)
Tiri tiri riri riri riri (tiriririri)
Upendo unanitiririka miee (tiriririri)
Tiririririri