Jux aachia albamu yake mpya 'King Of Hearts', umeipokeaje albamu hii?
Baada ya subira ya muda mrefu, hatimaye staa wa muziki wa R&B nchini Tanzania, Jux ameachia albamu ya 'King Of Hearts' ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Kwa muda mrefu, Jux amekuwa akidokeza ujio wa albamu hiyo kupitia mitandao ya kijamii na mahojiano mbalimbali ambayo amekuwa akifanya na mpaka kufikia hatua ya kuachia orodha ya nyimbo za albamu hiyo ya 'King Of Hearts'.
Katika albamu hiyo, imeshuhudiwa Jux akifanya kolabo na wasanii mahiri ndani na nje ya Tanzania kama vile wa Bien kutoka Kenya, Patoranking wa Nigeria, Mbosso wa WCB, Marioo, Zuchu katika ngoma ya 'Nidhibiti' na wakali wengine wengi wa muziki.
Ngoma zilizomo kwenye albamu hii ni 'Lucky Now', 'Sina Neno', 'Sing For You', 'I Love You', 'Mapepe', 'My Mind', 'Simuachi', 'Nidhibithi', 'Kitanda', 'Only You I See', 'Found Love', 'Number One', 'Wena', 'Show Dem', 'Sumu' na 'Nice (Kiss)'.
Vile vile 'Kings Of Hearts' inahusisha watayarishaji mahari wa muziki kama vile S2kizzy, Bob Manecky, Foxx Made It, Kapipo, Tony Duardo, Abbah Process na wengine.
< script async="" src="//www.instagram.com/embed.js"> script>
Hii ni albamu ya pili kutoka kwa Jux. Albamu yake ya kwanza inafahamika kwa jina la 'The Love Album' na ilimpa sifa na kuimarisha jina lake ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
#Music #Trending #Jux
Comments (3)
New Comments(3)
Irene Urban
BerryNipeys
Cool
JONAWISETZ
weka handle ✋ kwa Jux hapaaa[0x1f630][0x1f630][0x1f630][0x1f630][0x1f630][0x1f630][0x1f630][0x1f628][0x1f60e][0x1f60d][0x1f62e][0x1f62e][0x1f62e][0x1f62e][0x1f62e]
jux me napenda sana kazi zako [0x1f636][0x1f636][0x1f636]