Boom Milestone | 'Nitongoze' ya Rayvanny yafikisha streams milioni 1 Boomplay!
Ngoma ya mpya ya Rayvanny 'Nitongoze' imefanikiwa kufikisha streams milioni 1 kwenye jukwaa la Boomplay.
'Nitongoze' ni ngoma mpya ya Rayvanny ambayo aliiachia Ijumaa, Novemba 11, 2022 na mpaka sasa ni siku tano tu zimepita tangu kuachiwa.
Ngoma hii ya Amapiano ambayo amemshirikisha Diamond Platnumz ni moja ya ngoma kali ambazo Rayvanny amefanya na Diamond Platnumz. Ikumbukwe Rayvanny amewahi kuwa chini ya Diamond kupitia lebo ya WCB Wasafi.
Hii inakuwa ngoma ya sita wawili hawa kufanya pamoja. Ngoma nyingine ni 'Vumbi', 'Mwanza', 'Tetema', 'Amaboko', 'Iyena' na 'Salome'.
'Nitongoze' ni ngoma ambayo Rayvanny na Diamond wanasema kuwa jimbo liko wazi na yeyote anayewataka basi ruksa kuwatongoza.
"Hii ni sehemu ya mashairi ya wimbo huu: "Maswali mengi kwa waiter hauna hela nini (Eti), Iyo shingapi hii shingapi hauna hela nini (Eti), Maswali mengi kwa waiter hauna hela nini (Eti), Ile shingapi hii shingapi hauna hela nini, Nimeachwa sitaki tena maswali, Naenda beach kula upepo wa bahari, Naumwagilia moyo mziki kwa mbali, Jimbo likowazi sema nitakubali," Rayvanny.
"Ati unanitaka Eti unanipenda (basi nitongoze) Unanitaka Eti unanipenda (basi nitongoze) Unanitaka
Eti unanipenda (basi nitongoze) Unanitaka Eti unanipenda (basi nitongoze) Eh bwana we," Diamond Platnumz.
Ngoma hii imetayarishwa na moja ya watayarishaji mahiri kwa sasa Tanzania, S2Kizzy. Endelea kusikiliza 'Nitongoze' hapo chini kupitia Boomplay.
Nitongoze ft. Diamond Platnumz
#BuzzBrandColumn #BoomMilestone #Music #Trending #Nitongoze
Comments (40)
New Comments(40)
harimaselemani
Liliangpeqe
ok
nakupeda
152159922
ok nkukubli
Geofrey Elija
so cool
Engineerg0gb0
so lozenge
ericadzaz7
Nn Sasa……………awe…chiiiii
el paste officiel
hello family this is me El Paste From Congo
PASCHAL MWAMWEZI
iko bombaaaa
Romeo_ranx
Nice Chemistry wanatisha kila wakikutanaa
151304621
ngoma kali
Amina ie33f
wemkali
have